1 Kings 9:10-15

10 aMiaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alijenga majengo haya mawili, yaani Hekalu la Bwana na jumba la kifalme, 11 bMfalme Sulemani akampa Hiramu mfalme wa Tiro miji ishirini katika Galilaya, kwa sababu Hiramu alikuwa amempatia mierezi yote, misunobari na dhahabu yote aliyohitaji. 12 cLakini Hiramu alipotoka Tiro kwenda kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempa, hakupendezwa nayo. 13 dHiramu akauliza, “Hii ni miji ya namna gani uliyonipa, ndugu yangu?”

Naye akaiita nchi ya Kabul,
Kabul maana yake isiyofaa kitu.
jina lililoko hadi leo.
14 fBasi Hiramu alikuwa amempelekea mfalme talanta 120
Talanta 120 za dhahabu ni sawa na tani 4.5.
za dhahabu.

15 hHaya ni maelezo kuhusu kazi za kulazimishwa ambazo Mfalme Sulemani, alivyowafanyiza watu ili kulijenga hekalu la Bwana, na jumba la kifalme yake mwenyewe Milo,
Milo maana yake Boma la Ngome, pia 9:24.
ukuta wa Yerusalemu, Hazori, Megido na Gezeri.
Copyright information for SwhKC